Wakatamiwa wa Manungu mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar wameiweka Azam FC katika muendelezo wa kufukuzia ubingwa wa kwanza kwa Azam FC, baada ya kuvunja pambano la leo.
Mpambano huo ulivunjika katika dakika za lalasalama baada ya Mtibwa Sugar kugomea kwa kutoka nnje ya uwanja penati ya Azam FC waliyoipata katika dakika hizo kwa mchezaji wa Mtibwa Sugar kuunawa mpira huo katika eneo la hatari.
Katika mchezo huo Azam FC walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa mshambuliaji hatari nchini Mrisho Khalfan Ngassa kabla ya Mtibwa Sugar kusawazisha goli hilo kupitia kwa Salum Swed katika kipindi cha kwanza.
Katika kipindi cha pili mchezaji wa Mtibwa Sugar alizawadiwa kadi nyekundu, kabla ya mwamuzi huyo kuizawadia Azam FC mkwaju wa penati katika dakika za lalasalama, na kusababisha mpira kufunjika.
Kutokana na sheria ya ligi kuu ya vodacom, na Mtibwa Sugar kuwa ndio waliopelekea mpambano kuvunjika, Azam FC wamepewa ushindi wa goli 2-0 na hivyo kujihakikishia nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa kwa kufikisha point 53 ambazo haziwezwi kufikiwa na Yanga.
Monday, April 23, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment