Friday, July 13, 2012

Azam FC yapoteza fainali

Posted By: kj - 10:37 AM

Share

& Comment

Jana Usiku kwenye uwanja wa Taifa Simba SC ilitwaa ubingwa wa Kombe la Urafiki, baada ya kuifunga Azam FC kwa penalti 3-1 kufuatia timu zote kutoshana nguvu kwa kufungana 2-2 katika muda wa kawaida wa dakika 90.

(Pichani Juu Khamis Mcha Khamis, kinda mwenye umri wa miaka 21 ambaye alikuwa Nyota wa mchezo hapo jana.)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Sunzu alitangulia kuifungia Simba dakika ya 29 baada ya simba kupiga kona fupi na baadaye mpira kutua kichwani mwa Sunzu aliyefunga kwa kichwa lakini nyota wa mchezo wa jana Hamisi Mcha ‘Vialli’ alsawazisha dakika ya 45 kwa kichwa baada ya kuvunja mtego wa kuotea na kumhadaa golikipa wa Simba Juma Kaseja kwa ustadi mkubwa.

Katika kipindi cha pili cha mchezo, Azam FC ilifanya mabadiliko kadhaa kwa kuingia Aggrey Morris badala ya Joseph Owino, Jabir Aziz badala ya Kipre Bolou, Himid Mao badala ya Blackberry na John Bocco badala ya Kipre Tchetche mabadiliko yaliyofanywa ili kutoa nafasi za kupumzika kwa baadhi ya wachezaji kutokana ana timu kukabiliwa na Kagame Cup siku chache zijazo.

 Katika dakika ya 81, John Bocco ‘Adebayor’ aliyetokea benchi aliifungia Azam bao la pili kufuatia kona maridadi iliyochongwa na Mcha khamis.

 Wakati kila mtu akiamini kuwa mpira ungeisha kwa azam FC kushinda 2-1, Mwamuzi wa mchezo huo aliwazawadia simba Penati baada ya Dany Mrwanda kujiangusha kwenye eneo la hatari na penati hiyo ilipigwa na Mwinyi Kazimoto na kuisawazishia Simba katika dakika ya 87.



Penalti za Simba zilikwamishwa nyavuni na Mwinyi Kazomoto, Amir Maftah na Kiggi Makassy, wakati Haruna Moshi Boban alipaisha na kwa upande wa Azam FC, aliyefunga ni Hamisi Mcha ‘Vialli’ pekee, wakati Samir Hajji Nuhu ilidakwa na Juma Kaseja, Ibrahim Mwaipopo ilipanguliwa na Himid Mao ‘iliota mbawa’.

Azam FC; Deogratius Munishi, Ibrahim Shikanda, Simih Haji Nuhu, Jeseph Owino/Aggrey Morris, Said Moradi, Kipre Bolou/Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Ramadhan Chombo, George Odhiambo/Himid Mao, Kipre Tchetche/Jihn Bocco na Khamis Mcha Viali

Source: www.azamfc.co.tz

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.