Thursday, July 26, 2012

Azam hao Fainali wawangoja Yanga ama APR

Posted By: kj - 5:29 PM

Share

& Comment

Goli la Mrisho Khalfan Ngassa katika dakika za majerehu lilitosha kuipeleka Azam FC fainali ya michuano ya kombe la Kagame litakalochezwa siku ya jumamosi (julai 28) katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo ulioanza saa 8 mchana katika uwanja wa Taifa, Azam FC waliuwanza vyema mchezo kwa kutandaza mpira chini ambao unatumiwa pia na wapinzani wao wa leo AS Vita ya DR Congo ambao leo walijaza viungo wengi kati, kitendo kilichopelekea kumiliki na kupandisha mashambulizi na mchezo huo kuwa sawa kwa pande zote mbili katika kipindi cha kwanza.

Katika dakika ya 33 AS Vita walitumia vyema makosa ya beki ya Azam na kufunga goli la kuongoza lililo tiwa kimiani na Affrey, goli hilo liliwaamsha Azam FC na kuanza kusaka goli la kusawazisha.

Kaikta dakika ya 38 beki wa AS Vita Isama Mpetu alizawadiwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya manjano na kupelekea AS Vita kumaliza wakiwa pungufu mchezaji mmoja.

Katika kipindi cha pili Azam FC walianza kwa kufanya mabadiliko ya kutoka Jabir Azizi na nafasi yake kuchukuliwa na Mrisho Ngassa, mabadiliko hayo yalipelekea Azam FC kulisakama lango la AS Vita bila mafanikio mpaka pale kocha Stewart Hall kufanya mabadiliko mengine ya kumtoa Ibrahim Shikanda na nafasi yake kuingia Samir Haji Nuhu.

Mabadiliko hayo yalipelekea Erasto Nyoni kurejea kwenye upande wa kulia na katika dakika ya 68 alipiga krosi iliyomkuta John Bocco, ambapo bila ajizi aliisawazishia Azam huku akifunga goli lake la 5 katika michuano hiyo na kubakisha goli moja kumfikia kinara wa magoli Taddy wa AS Vita mwenye magoli 6.

Hall alimpumzisha Kipre Tchetche na kumuingiza Gaudence Mwaikimba mabadiliko ambayo yalifanya Azam kuzidisha presha katika lango la AS Vita.

Katika dakika ya 88 SalumAboubakari alikokta mpira kutokea na kulikaribia penati area ya AS Vita na kumgusia Mrisho Ngassa ambapo bila ajizi aliifungia Azam FC goli la pili.

Katika dakika ya mwisho Mrisho Ngassa nusura aiandikie Azam goli la 3 alipo baki na kipa katika shambulio la kushtukiza ambapo beki wa AS Vita aliuwahi mpira kabla ya kuvuka mstari wa goli na mpira kumalizika kwa ushundi wa goli 2-1.

Azam FC watacheza na mshindi kati ya Yanga na APR katika mchezo wa fainali, na mpaka post hii inaandikwa matokeo yalikuwa 0-0 dakika ya 57.
2-1 AS VITA (BOCCO 68, NGASSA 88; AFFREY 33)

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.