Mabingwa wa michuano ya kombe la Mapinduzi Azam FC watakutana na Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Simba SC katika mchezo wa fainali wa kombe la urafiki utakao pigwa hapo kesho katika uwanja wa Amani Zanzibar.
Mabao mawili ya mshambujliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Herman Tcheche, jioni ya jana yalitosha kuipeleka Azam FC katika hatua ya Fainali kabla ya Simba SC kufanya hivyo katika usiku wa jana kwa kuifunga All Stars goli 1-0.
Azam FC na Super Falcon zilienda mapumzi bila ya kufungana, na kipindi cha pili kilianza vibaya kwa Azam FC baada ya Mshambuliaji mwenye mwili mkubwa Gaudence Exavery Mwakimba kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika dakika ya 54 kwa kumpiga kiwiko Abdul Ally.
Goli la kwanza la Azam FC lilipatika katika dakika ya 67 baada ya Kipre Tcheche kabla ya kuhitimisha kwa kufunga goli la pili kwa mkwaju wa penalti, katika dakika ya 77, baada ya Samir Haji Nuhu kuangushwa kwenye eneo la hatari na Samir Said.
Simba SC na Azam FC walikutana katika hatua ya makundi ambapo Azam FC wakiwa pungufu takribani kipindi chote cha pili, waliwazibiti Simba SC na kutoka sare ya bila kufungana.
Kikosi cha Azam kilicho ifunga goli 2-0 Falcon kiliundwa na: Deo Munishi ‘Dida’, Samir Hajji Nuhu, Ibrahim Shikanda, Said Mourad, Joseph Owino, Ibrahim Mwaipopo/Himid Mao Mkami, Kipre Herman Tcheche/Hamisi Mcha, Kipre Michael Balou/Abdulhalim Humud, Ramadhan Chombo ‘Redondo’, Gaudence Mwaikimba na George Odhiambo ‘Blackberry’/Zahor Pazi.
Tuesday, July 10, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment