Tuesday, August 28, 2012

Odhiambo kutovaa uzi wa Azam

Posted By: kj - 7:54 AM

Share

& Comment


Mabingwa wa kombe la Mapinduzi na washindi wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara, Azam FC wamesitisha mkataba na mshambuliaji wao toka Kenya George Odhiambo 'Blackberry' kutokana na ukuikwaji wa mkataba uliofanywa na mshambuliaji huyo.

Msemaji wa Azam FC amesema kuwa mshambuliaji huyo toka Kenya amekeuka mkataba wake na Azam FC, hivyo uongozi wa Azam FC uliona huna budi kumuondoa mchezaji huyo kwa kitendo alicho kifanya.

Odhiambo aliingia mkataba na Azam FC kwa ajili ya msimu utakao funguliwa september mosi kwa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Azam FC na Simba SC pamoja na kombe la shirikisho mwakani.

Mpaka mkataba wake unasitishwa, Odhiambo alikuwa bado haja jihakikishia namba katika kikosi cha kwanza cha Azam FC.


SNURCE: SPORT IN BONGO

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.