Saturday, December 22, 2012

MSUNI ANGOJA ZAWADI YA UBINGWA TOKA AZAM

Posted By: kj - 7:34 AM

Share

& Comment

Bogger wa Azam Fans Club na mmiliki wa Aboodmsuni Network 'AN' Abdallah H.I Sulayman 'Msuni' jana alifinga ndoa na Bashira mjini Morogoro wakati vikosi vya Azam Academy na Azam FC zikikata tiketi ya kutinga fainali karika michuano inayoshiriki.

Academy waliwafunga Mtibwa sugar kwa mikwahu ya penati 4-3 baada ya kumaliza mchezo wakiwa sare ya goli 1-1 katika nusu fainali ya kwanza ya Uhai Cup iliyochezwa asubuhi kabla ya kaka zao kushinda kw penati 5-4, baada ya kutoka sare ya goli 2-2.

Fainali zote zitachezwa kesho jumaplili december 23, wakati Academy wakicheza na Coastal Union katika uwamja wa Karume jijini Dar es salaam wakati kaka zao watakuwa DRC.


KUTOKA KWA BIN ZUBEIRY
Kipa Mwadini Ally kulia akimpongeza Nahodha wake, Jabir Aziz baada ya kufunga penalti ya mwisho

Na Mahmoud Zubeiry, Kinshasa
AZAM FC imefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Hisani, baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penalti 5-4 Shark FC ya hapa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs jioni hii.
Nahodha Jabir Aziz Stima ndiye aliyekwenda kupiga penalti ya mwisho, Shark wakitoka kupoteza, kufuatia mpira kugonga mwamba. Aiziz aliwainua vitini wachezaji wenzake na makocha wake pamoja na viongozi wa wachache wa timu hiyo waliopo hapa kwa kupiga penalti maridadi iliyotinga nyavuni.
Azam sasa, itamenyana na mshindi wa mechi inayoendelea hivi sasa kati ya Dragons na FC MK Jumapili katika fainali.
Azam iliuanza mchezo huo vizuri na ikicheza kwa maelewano makubwa sambamba na kushambulia kwa kasi kutokea pembeni, kulia Kipre Herman Tchetche na kushoto Seif Abdallah.
Hata hivyo, shambulizi la kushitukiza la Shark liliwapa bao la kuongoza dakika ya 16, lililofungwa na Ngulubi Kilua, baada ya mabeki wa Azam kudhani ameotea.
Iliwachukua dakika 10 tu Azam kusawazisha bao hilo, mfungaji akiwa Gaudence Exavery Mwaikimba aliyeunganisha kwa kichwa krosi maridadi ya nyota wa mchezo wa leo, Kipere Herman Tcheche kutoka wingi ya kulia.
Baada ya bao hilo, Azam iliendelea kuwashambulia Shark na dakika ya 37, Kipre Tchetche aliifungia timu hiyo bao la pili, kufuatia kazi nzuri ya Mwaikimba. Mwaikimba alipokea mpira mrefu, akatuliza na kumtangulizia kwa mbele mfungaji, ambaye hakufanya makosa, alimchambua kipa wa timu inayomilikiwa na mdogo wa rais wa DRC, Joseph Kabila.       
Hadi mapumziko, Azam ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-1 na kipindi cha pili Shark waliingia kwa kasi na kufanikiwa kusawazisha kwa penalti dakika ya 47, iliyotiwa nyavuni na Bukasa Kalambai, ambaye yeye mwenyewe alijiangusha kwenye eneo la hatari baada ya kuzongwa na beki David Mwantika.
Baada ya dakika 90 kutimu timu hizo zikiwa zimefungana 2-2, sheria ya matuta ilichukua mkondo wake na wachezaji wote watano wa Azam waliopewa dhamana hiyo leo na kocha Muingereza Stewart Hall, walitimiza wajibu wao vizuri.
Kipre Tchetche alifunga ya kwanza, Mwaikimba ya pili, Jaockins Atudo ya tatu, Himid Mao ya nne na Stima akapiga ya ushindi.
Stewart alisema amefurahishwa na matokeo ya mchezo wa leo na sasa ana matumaini ya timu yake kurejea na Kombe hilo Dar es Salaam.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Azam kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samih Hajji Nuhu, Joackins Atudo, David Mwantika, Jabir Aziz, Kipre Balou, Seif Abdallah/Uhuru Suleiman dk 77, Kipre Tchetche, Humphrey Mieno na Gaudence Mwaikimba. 

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.