Sunday, January 6, 2013

AZAM WANUSA NUSU, WAICHAPA GOLI 3 MIEMBENI

Posted By: azam fans - 7:04 AM

Share

& Comment

Azam fc wamenusa nusu fainali ya kombe la mapinduzi baada ya kuwafunga Miembeni goli 3-1 katika mchezo tlichezwa hapo jana usiku wa kundi B.

Katika mchezo wa huoi uliowakutanisha makocha wazamani wa Zanzibar heroes walio fanikisha kuifikisha nusu fainali ya chelenge cup Salum Bausi wa miembeni na Stewart Hall wa azam fc na kushuhudia makocha wote wakitolewa kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumzonga mwamuzi wakati timu zikielekea mapumzikoni waki mlalamikia kushindwa kumudu pambano hilo.

Azam walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 2 kupitia kwa mkenya Juackin Akudo akiunga kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Humphrey Mfuno.

Goli hilo halikudumu kwani katika dakika ya 4 Adeyoum Saleh aliisawazishia miembeni kwa mpira wa kona uliotinga moja kwa moja nyavuni kabla ya Gaudency Mwaikimba kuipatia goli lapili azam katika dakika ya 34 na Uhuru Seldmani kuhitimisha katika dakika ya 87.

Kwa matokeo ya jana Azam wanaongoza kundi kwa kuwa na point 4 wakifuatiwa na Miembeni wenye point 3, Coastal union wakiwa na 2 na Mtibwa sugar wenye point moja.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.