Monday, April 14, 2014

AZAM FC YABAKIZA MICHEZO 16 KUFIKISHA RIKODI YA ARSENAL

Posted By: kj - 8:29 PM

Share

& Comment

Zaka Zakazi
Azam wameweka rekodi ya kucheza mechi nyingi za ligi kuu bila kupoteza, mpaka sasa wamecheza mechi 33. Mara ya mwisho kupoteza mchezo wa ligi kuu ilikuwa Februari 23, 2013(msimu wa 2012-13) walipofungwa 1-0 na Yanga. Huo ulikuwa mchezo wa 18, ilibaki michezo 8 ligi iishe. Msimu huu mpaka sasa wamecheza mechi 25 pasipo kupoteza, jumla inakuwa michezo 33. Rekodi hii hapo kabla ilikuwa ikishikiliwa na Simba SC ambao walicheza mechi 30 pasipo kupoteza. Mara ya mwisho Simba walifungwa 1-0 na Mtibwa March 22, 2009(msimu wa 2008-09). Ulikuwa mchezo wa 17, ikiwa imebaki michezo 4(wakati huo ligi ilikuwa na timu 12). Baada ya hapo, Simba walimaliza msimu wa 2009-10 pasipo kupoteza, wakicheza mechi 22. Rekodi yao ilkaishia Septemba 19, 2010 walipofungwa na Polisi Dodoma. Ulikuwa mchezo wa 4 tokea ligi ianze.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.