HAKUNA dhambi yoyote kwa Azam kuchukua ubingwa. Sijaiona dhambi hiyo bado. Kama unaweza kucheza mechi 25 kati ya 26 na bado haujafungwa mechi hata moja basi una kitu cha ziada zaidi kuliko wapinzani wako.
Kuna maneno ya chini chini kwamba huenda Azam
imefanya hujuma za hapa na pale katika kupata ubingwa. Lakini ukweli
unabaki pale pale kwamba Azam ilistahili kutwaa ubingwa kwa sababu
zifuatazo.
Wamecheza mechi nne dhidi ya Simba na Yanga katika
Uwanja wa Taifa. Mbele ya mashabiki wanaomzomea Kipre Tchetche na
wachezaji wote wengine wa timu hiyo. Lakini pamoja na kelele hizo Azam
imepoteza pointi mbili tu za sare yao ya pambano la pili dhidi ya Yanga.
Wameichapa Simba mara mbili. Wameichapa Yanga mara
moja. Wametoka sare moja na Yanga. Kwanini nimetoa mfano wa Simba na
Yanga tu? Kwa sababu mashabiki wa timu hizi mbili wanaamini kwamba wao
tu ndio timu zao zinastahili kuwa mabingwa.
Lakini hizi mbili za Dar es salaam ndio zina
matumizi makubwa ya pesa katika dirisha la uhamisho. Ndizo timu ambazo
katika magazeti zinaongoza kwa kufanya usajili wa mamilioni nchini. Kama
unaweza kucheza nazo mechi nne mbele ya mashabiki wao na washindwe
kukufunga ujue kuna kitu cha ziada kipo.
Hata hivyo, hakuna dhambi kwa Azam kuchukua
ubingwa kwa sababu Simba ilijifuta katika mbio za ubingwa kabla ya
kuanza kwa Ligi Kuu Bara. Walifanya usajili mara tatu ndani ya dirisha
moja wakianzia usajili ule wa kitoto walioufanya kwa kusajili wachezaji
watoto watupu.
Niliwahi kuandika katika makala moja kwamba aina
ya usajili wa Simba ungeziacha Azam na Yanga zikiwania ubingwa. Na kweli
hawakufika mbali. Wachezaji wao makinda wakakata pumzi mwishowe akabaki
Amiss Tambwe peke yake.
Yanga walikuwa na timu nzuri, lakini kama ilivyo
kawaida kwao, walitibuana kila wiki. Wachezaji watano au sita
walishutumiwa kuhujumu timu kwa nyakati tofauti ukianzia kwa Ally
Mustapha ‘Barthez’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani, Juma
Kaseja, Athuman Idd, Emmanuel Okwi na wengineo.
Waliporudi kutoka Al Alhy walikuwa wamevimba kichwa na jinsi walivyocheza mechi zao mbili vizuri.
Hawakuweza kujipanga tena kucheza vizuri mechi za
ndani ambazo zilikuwa muhimu sana kwao ili warudi tena michuano ya
Afrika msimu ujao.
Yanga ndio timu yenye kikosi bora pengine kuliko
Azam. Lakini mpira hauchezwi katika magazeti. Wakati Azam wakijipanga
kimya kimya kwa kuua wapinzani wao kwenye Uwanja wa Chamazi na ugenini,
Yanga walitumia muda mwingi kulumbana wenyewe kwa wenyewe.
Kifupi Simba na Yanga zinapokuwa katika hali hii,
halafu kuna timu iliyowekeza pesa vizuri na yenye matunzo kwa wachezaji
wake, ni rahisi tu kutwaa ubingwa. Tatizo letu tumekariri kwa sababu
wakati mwingine timu hizi zinatwaa mataji zikiwa na vikosi vibovu
kutokana na ubovu wa timu nyingine.
Ubovu wa vikosi vya Manchester United na Arsenal ulionekana papo
hapo mara Jose Mourinho alipokuja England na kuanza kushinda mataji kwa
pesa za Roman Abramovich. Sir Alex Ferguson walau alijirekebisha,
lakini Arsene Wenger akabakia kuwa jiwe na mbinu zake za zamani.
Na ndicho kinachotokea Tanzania kwa sasa. Hakuna tofauti sana
0 Maoni:
Post a Comment