Tuesday, April 29, 2014

KAVUMBAGU KUVAA UZI WA AZAM MSIMU UJAO

Posted By: kj - 4:58 PM

Share

& Comment

Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
NAHODHA wa Burundi, Didier Kavumbangu amesaini Mkataba wa miaka miwili na mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC mchana wa leo, BIN ZUBEIRY imeipata hiyo.
Kavumbangu aliyemaliza Mkataba wake wa miaka miwili Yanga SC, ameamua kusaini Azam FC baada ya kuona klabu yake haina mawasiliano naye licha ya kumaliza Mkataba wake.
“Mimi ni mchezaji, kazi yangu ni mpira. Nimemaliza mkataba Yanga, lakini viongozi hawaniambii kitu, nimepata ofa nzuri Azam nikaamua kusaini,” amesema Kavumbangu akizungumza na BIN ZUBEIRY baada ya kusaini Mkataba huo ambao unamfanya alipwe vizuri kuliko alivyokuwa analipwa Jangwani.
Maisha mapya; Kavumbangu akitia dole gomba Mkataba wa Azam leo

Pamoja na hayo, Kavumbangu ameishukuru Yanga SC na mashabiki kwa miaka miwili aliyoichezea timu hiyo na anasema itabakia kwenye kumbukumbu zake kwa ameshinda nayo mataji.
Mshambuliaji huyo mrefu mwenye nguvu amesema sasa akili yake anaipeleka kwa mwajiri wake mpya, Azam FC ambako pia amepania kwenda kushinda mataji na kuiwezesha timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika.  
“Mimi sasa ni mchezaji wa Azam, nafurahi kujiunga na klabu hii kubwa. Kawaida yangu huwa nashabikia klabu nayochezea, sasa mimi ni mshabiki namba moja wa Azam,”amesema.   
Tukutane Chamazi; Kavumbangu anahamisha virago vyake kutoka Jangwnai hadi Chamazi

Kavumbangu alitua Yanga mwaka 2013 akitokea Atletico ya Burundi na katika mechi misimu miwili ya kuichezea klabu hiyo, amefunga mabao 31 katika mechi 63 za mashindano yote, moja tu lA PENATI

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.