KAZI ipo mwaka huu, Azam FC inazidi kutamba na sasa Kocha wake
Joseph Omog ametamka wazi kuwa, licha ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara
msimu uliopita, wachezaji wake walikuwa na nidhamu ndogo ya mpira, hivyo
amejiandaa kuwapa mbinu kali kama zinazotumiwa na TP Mazembe ili waende
sawa katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
Omog alisema: “Nidhamu ya ndani ya uwanja
ninayozungumzia hapa ni ile tabia ya kutofautiana na mwamuzi au
wachezaji wa timu pinzani kwa kujibizana nao au kugombana
wanapotofautiana. Hilo si jambo la kimichezo linaweza kuiathiri timu
wakati wowote na mimi kama kocha, sitaki kuona mchezaji wangu
anagombana.
“Ukiwa mchezaji wa kulipwa lazima utambue kazi
yako uwanjani ni kucheza mpira tu na hutakiwi kubishana au kugombana na
timu pinzani au mwamuzi bila sababu, wapo wahusika watalifanyia kazi,
huwa sipendi kabisa tabia hiyo,” alisema Omog.
“Huo ndiyo mpira wa kisasa unaochezwa na timu
kubwa zenye mafanikio kama TP Mazembe na nyinginezo duniani nami nataka
timu yangu iwe hivyo kwa sababu tunakwenda kushiriki mashindano makubwa
ya ligi ya Mabingwa na kukutana na timu za mataifa mbalimbali,”
alifafanua.
CHANZO: MWANASPOTI
CHANZO: MWANASPOTI
0 Maoni:
Post a Comment