Tuesday, September 23, 2014

AZAM FC WAANZA KUWAVUTIA KASI RUVU SHOOTING

Posted By: kj - 7:11 PM

Share

& Comment


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgm0ttktuyABRphj-cSa17A2iPONwljKMmew7IpRnrZ4nu3npaEzp02U9m0xgOeAg5-ycAXbnpYDd31rFOgMqXXVLXuGhKqk7qpYaTTdFmxe5MRVxgUmLws9oTRhMaKy_lgfkjLWlqIHPxG/s1600/3.jpg

Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara Azam FC wameingia kambini jioni ya leo teyari kwa maandalizi ya kuwakabili Ruvu shooting katika mchezo wa pili wa ligi kuu Tanzania bara utakao chezwa jumamosi ya wki hii katik uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Azam FC ambayo imeichapa Polisi Morogoro goli 3-1 katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu, wameanza mazoezi jioni ya leo kueleka mchezo huo wa juma mosi.

Msimu uliopita Azam FC walifanikiwa kuvuna pointi zote 6 kwa Ruvu shooting baada ya kuwafunga katika michezo yote miwili waliyo kutana katika msimu uliopita uliomalizika kwa Azam FC kutwaa ubingwa wa Tanzania bara bila ya kupoteza mchezo wowote ule.

Ruvu shooting katika mchezo wao wa ufunguzi wa ligi kuu ya vodacom msimu wa 2014/15 wamekubali kichapo cha goli 2-0 toka kwa Tanzania Prisons mchezo uliochezwa katika uwanja wa Ruvu shooting (Mabatini) uliopo Pwani.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.