Sunday, December 14, 2014

AZAM WAANZA VIBAYA ZIARA YAO UGANDA

Posted By: Unknown - 10:48 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara Azam fc hii leo wamekubali kichapo cha goli 3-2 toka kwa SC Villa ya Uganda katika mchezo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa Navigubo nchini Uganda.

Katika mchezo huo wa kwanza wa kirafiki kwa azam fc nchini Uganda, azam fc ndio walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Didier Kavumbagu akiunga krosi ya Khamisi Mcha katika dakika ya 5.

SC Villa walisawazisha kupitia kwa Mkata Fredi katika dakika ya 42 na kupelekea mchezo kwenda mapumziko kwa sare ya goli 1-1.

Katika kipindi cha pili azam fc walitangulia kupata goli la pili kupitia kwa Khamis Mcha kwa mpira wa faulo, ikiwa ni kabla ya SC Villa kuandika goli la pili na la tatu na kupelekea mchezo kumalizika kwa sc villa kuibuka na ushindi wa goli 3-2.

Kikosi kilichoanza leo: Mwadini Ally, Shomari Kapombe, Gardiel Michael, Pascal Wawa, Agrey Morice, Kipre Bolou, Khamis Mcha, Mudathir Yahya, Kavumbagu, Kiemba na Himid Mao

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.