![]() |
Wawa akiwasili Dar |
Beki mpya wa Azam FC raia wa Ivory coast, Pascal Wawa ametua leo asubuhi akitokea nchini Ivory cxoast teyari kuanza kibarua kipya katika kikosi cha mabingwa wa Tanzania Bara Azam FC.
Wawa amesajiliwa Azam FC akitokea kwa El-merekh ya Sudan baada ya kumaliza mkataba wake na El-merekh ambapo ameingia na Azam FC mkataba wa mwaka mmoja.
Wawa ambaye alifanya vyema katika kiosi cha El merekh wakati wa michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati iliyofanyika nchini Rwanda na El-mereikh kuibuka bingwa wa michuano hiyo.
Uongozi wa Azam FC na mashabiki wake wanaimani na Wawa kuwa atatoa mchango mkubwa kwa Azam FC katika safari yake ya kushiriki kwa mara ya kwanza klabu bingwa Afrika ambapo Wawa amefanya hiyvo mara kadhaa akiwa na El-mereikh.
Wakati Wawa akiwasili leo Muivory coast mwingine anae kipiga Azam FC Kipre Herman Tcheche anatarajiwa kuwasili kesho teyari kwa kuanza maandalizi ya kujiandaa na michezo ya ligi kuu ya vodacom sambamba na klabu bingwa Afrika.
Azam FC wanaendelea na mazoezi ya kusaka makali katika uwanja wake wa Azam Complex huku kukiwa na taarifa ya Azam FC kwenda Zambia kucheza michezo kadhaa ya kirafiki kabla ya ligi kuu kuendelea hapo desemba 26 mwaka huu.
0 Maoni:
Post a Comment