Thursday, January 29, 2015

AZAM FC HUENDA WAKACHEZA NA FC LUPOPO KABLA YA KUREJEA

Posted By: Unknown - 11:27 AM

Share

& Comment

http://www.kigalitoday.com/IMG/jpg/Sina_uwa_gatatu_uturutse_ibumoso_yari_amaze_iminsi_akina_muri_FC_Lupopo_muri_Congo-.jpg
Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara Azam FC huenda ikacheza na FC Lupopo ya DR Congo kabla ya kurejea nchini februari 4 kwa ajili ya muendelezo wa ligi kuu ya Tanzania bara na mchezo wa klabu bingwa Afrika dhidi ya El-merekh.

Azam FC ambayo ipo DR Congo wameobwa na FC Lupopo kucheza mchezo wa kirafiki baada ya michuano maalum ya TP Mazembe yaliyoanza jana kumalizika.
 
“Nadhani Lupopo wamevutiwa na sisi, wameomba tucheze nao lakini bado hatujaamua itakuwa lini,” alisema Meneja wa Azam FC Jemedari Saidi.

Azam FC jana imecheza mchezo wake wa kwanza kati ya mitatu itakayo cheza katika mashindano hayo mafupi yaliyo andaliwa na TP Mazembe, ambao Azam FC walikubali kufungwa goli 1-0 dhidi ya wenyeji wao TP Mazembe.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.