Tuesday, January 27, 2015

AZAM FC KUFUNGUA NA TP MAZEMBE KESHO, LIVE AZAM TV

Posted By: Unknown - 3:58 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara Azam FC wamewasili salama nchini DR Congo teyari kwa mashindano mafupi yaliyoandaliwa na timu ya TP Mazembe ya nchini humo.

Katika michuano hiyo inayotaraji kuanza kesho na kufikia tamati februari 3 mwaka huu yatashirikisha timu nne ambao ni Azam FC, TP Mazembe, Don Bosco na Zesco ya Zambia.

Azam FC kesho saa kumi na moja jioni kwa masaa ya Tanzania sawa na saa kumi  kamili kwa masaa ya DR Congo, watacheza dhidi ya TP Mazembe ukitanguliwa na mchezo kati ya ZESCO na Don Bosco.

Azam FC waliondoka alfajiri ya leo kuelekea DR Congo ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa katika ukurasa wa azam fc unasema wamewasili salama. 'Kikosi cha Azam FC kimetua salama Lubumbashi DRC na Kenya Airways.' ilieleza taarifa hiyo iliyopo ndani ya ukurasa wa Azam FC wa facebook.

Katika hatua nyingine kitua cha telvisheni cha Azam TV kitaonyesha michezo hiyo kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye ukurasa wa Azam FC.

'Azam FC itatua dimbani kesho Jumatano Tarehe 28 kukwaana na TP Mazembe, mechi itaanza saa 11 Jioni kwa saa za Tanzania. Huku DRC itakuwa saa 10 Jioni. Mechi zote zitakuwa Live Azam TV,' ilieleza taarifa hiyo

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.