Monday, March 9, 2015

KAVUMBAGU AHIDI MAKUBWA CHAMANZI

Posted By: kj - 4:01 PM

Share

& Comment

Mshambuliaji wa Azam, Didier Kavumbagu, amesema anajisikia furaha kuona kiwango chake kinazidi kupanda tangu ajiunge na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.

Kavumbagu ambaye alitua Azam mwaka jana akitokea Yanga, juzi aliifungia timu yake bao pekee dhidi ya JKT Ruvu na kuifanya ifikishe pointi 30 hivyo kuendelea kukaa katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kavumbagu, alisema malengo yake ni kuona Azam inafanikiwa kutetea ubingwa na endapo naye atatwaa kiatu cha dhahabu, atafurahia zaidi.

Alisema ushindi wa timu ndiyo ni jambo muhimu na tuzo kwa mchezaji mmoja mmoja ndiyo zifuatie.

"Nafurahi kufanya vizuri, inanijenga na inaiweka timu yangu katika nafasi nzuri, bado naendelea kumuomba Mungu," alisema kwa kifupi mshambuliaji huyo ambaye ni raia wa Burundi.

Aliongeza kwamba bado anataka kuona juhudi zake na mchango wake pia anautoa na kwenye timu yake ya Taifa ya Burundi.

Licha ya kutolewa na El Merreikh katika mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Azam pia mwaka huu itashiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) ambayo hufanyika kati ya Mei na Juni kila mwaka chini ya Cecafa.

CHANZO: NIPASHE

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.