Saturday, March 7, 2015

KAVUMBAGU AIPA USHINDI AZAM FC, SURE BOY AKIPEWA KADI NYEKUNDU

Posted By: kj - 7:30 PM

Share

& Comment

Goli la pekee la mshambuliaji wa Azam FC toka Burundi Didier Kavumbagu lilitosha kuwapa point tatu muhimu Azam FC mbele ya JKT Ruvu, mchezo uliochezwa katika uwanja wa Azam Complex. Goli hilo lilikuwa la tisa kwa Kavumbagu msimu huu.

Katika mchezo huo ambao umeshuhudia kadi mbili nyekundu zikitolewa kwa upande zote mbili, Azam FC waliandika goli la kuongoza katika dakika ya 16 kupitia kwa Kavumbagu akiunga krosi ya Shomari Kapombe.

Kuingia kwa goli hilo lilipelekea Azam FC kuutawala mchezo na kutengeneza nafasi kadha za kuandika magoli, na kama Kipre Tcheche na Brian Majegwa wangeenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli zaidi ya matatu.

Kipindi cha pili JKT Ruvu walirejea kwa kasi na kupelekea Azam FC muda mwingi kupoteza katika kusaka mpira na kupeleka mashambulizi ya kushtukiza.

Katika dakika ya 58 kiungo wa Azam FC Salum Aboubakari na mchezaji wa JKT Ruvu Richard Manyara walizawadia kadi nyekundu, na kupeleka upepo wa mchezo kubadilika.

Azam FC walianza kucheza pasi nyingi kila wanapo pata mpira huku JKT Ruvu wakipambana kusaka goli la kusawazisha na kupelekea mchezo kumalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.