Katibu mkuu wa Azam FC Nassor Saidi amesema kuwa Hall ni miongoni mwa makocha watatu wanao fanya nao mazungumzo na mwishoni mwajuma hili ama mwanzoni mwajuma lijalo wataweka hadharani kocha atakae ifundisha kikosi hicho.
Nassoro alisema kuwa maongezi yanakwenda vyema na makocha hao watatu, ambao wamepeleka wenyewe maombi ya kuifundisha Azam FC, akiwemo na Hall.
Hall kwa mara ya kwanza alijiunga na Azam FC katika msimu wa 2010/11 na kuiwezesha Azam FC kushika nafasi ya pili na mwaka 2011 kuiongoza Azam FC katika fainali ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati (Kagame Cup).
Hall alirejea Azam fc katika mzunguko wa pili wa msimu 2011/12 na kuiwezesha Azam Fc kushika nafasi ya pili kwa mara ya pili mfululizo huku katika kombe la shirikisho ikiishia katika raundi ya pili.
SIB 90
POPULAR
TAGS
0 Maoni:
Post a Comment