Wednesday, May 13, 2015

MORAD, NYONI WAPEWA MIKATABA AZAM FC

Posted By: Unknown - 8:58 PM

Share

& Comment

Uongozi wa Azam FC umezima ndoto ya Simba SC kumrejesha kikosini mwao beki Saidi Morad, baada ya kumpatia mkataba mpya wa kutiumikia Azam FC.

Moradi aliyejiunga na Azam FC akitokea Kagera sugar mkataba wake ulimalizika mwezi machi sambamba na beki Erasto Nyoni.

Msemaji wa Azam FC Japhari Iddi amesema kuwa Azam FC imewaongezea mkataba wachezaji wake watatu ambao mikataba yao imekuwa imekwisha ambao ni Said Moradi, Erasto Nyoni na Didier Kavumbagu.

Japhari alisema kuwa kumalizika kwa mikataba ya Erasto na Morad kulisababisha kukosekana kwao katika michezo ya mwisho ya ligi.

Morad amekuwa akihusishwa na kurejea Simba SC kabla ya kusaini mkataba, mpya wa kuitumikia Azam.

Morad alipata kupitia Simba kabla ya kujiunga na Kagera sugar, ambapo Simba walimchukuwa kutoka Ashanti united ya Ilala jijini Dar es salaam.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.