
Kikosi hicho cha Azam kinachonolewa na Muingereza, Stewart Hall, mpaka sasa bado hakijaanza harakati za usajili ukilinganisha na timu za Simba na Yanga ambazo mpaka sasa tayari zimeshasajili wachezaji zaidi ya wane kila moja.
Msemaji wa kikosi hicho, Jaffar Idd Maganga, alisema kuwa licha za wapinzani wao Simba na Yanga kuanza harakati za usajili, wao hawana haraka na jambo hilo, badala yake wanajipanga ili kuweza kufanya usajili makini na kwenye nafasi ambazo zina mapengo.
“Sisi kwa upande wetu wala hatuna shida ya kufanya usajili wa haraka kama baadhi ya timu zilivyoanza jambo hilo, badala yake tunajipanga tu huku tukisubiri muda ufike ndiyo tuanze kufanya hivyo.
“Usajili wetu utajikita zaidi katika maelekezo ya ripoti ambayo iliachwa na kocha ambapo tutasajili kulingana na nafasi ambazo tumeona zinahitaji kuongezewa nguvu,” alisema Maganga.
CHANZO: salehjembe.blogspot.com
SIB 90
POPULAR
TAGS
0 Maoni:
Post a Comment