Wednesday, July 15, 2015

MIGI APEWA MIAKA MIWILI AZAM FC, KUJIUNGA NA TIMU TENA BAADA YA KAGAME

Posted By: kj - 6:28 AM

Share

& Comment

Kiungo wa kimataifa wa Rwanda Jean Baptiste Mugiraneza 'Migi' amesaini mkataba wa kutitumikia Azam FC wa miaka miwili baada ya kufanya vyema katika majaribio yake ya siku 5.

Migi alitua nchini siku ya jumatano na kujiunga na Azam FC moja kwa moja katika mazoezi ya Azam FC na kufanikiwa kucheza michezo miwili ya Kirafiki dhidi ya Coastal Union na African Sport ambapo Azam FC walishinda kwa goli 1-0 katika michezo yote waliyo cheza.

Migi anakuwa mchezaji wa 6 wakigeni katika kikosi cha Azam FC na kufanya ibakie nafasi moja ambayo itakuwa inawaniwa na wachezaji wanne waliopo Chamanzi kwa ajili ya majaribio, ambapo nafasi kubwa ya kujaza nafasi hiyo anapewa Muingereza Ryan Burge.

Migi anatajiunga na timu yake ya APR katika michuano ya kombe la Kagame kabla ya kurejea kuitumikia rasmi Azam FC baada ya michuano hiyo inayoanza jumamosi kumalizika.

Wachezaji wengine wanao saka nafasi hiyo moja ya kusajiliwa na Azam FC ni pamoja na  Nelson Lukong kutoka Cameroon, Vincent Atchouailou de Paul Angban kutoka Ivory Coast na Allan Wetende Wanga kutoka Kenya.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.