Kiungo wa Azam FC Jean Mugiraneza ‘Migi’ amejiunga na timu hiyo hivi karibuni akitokea APR FC ya Rwanda na kufanikiwa kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo ambapo aliisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa Kagame kwa kuifunga timu ya Gor Mahia ya Kenya kwa goli 2-0.
Migi ametoboa siri ya yeye kumudu kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Azam alipofanya mahojiano na mtandao huu mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali huku akianza kwa kuelezea furaha yake kwa kutwaa ubingwa huo ambao alishacheza fainali mbili na kuukosa hatimaye akafanikiwa kunyanyua kombe hilo kwenye fainali yake ya tatu akiwa na Azam FC.
Swali: Hii ilikuwa ni fainali yako ya tatu kwenye michuano ya Kagame umekosa kombe mara mbili lakini safari hii umefanikikiwa kushinda ukiwa Azam, unajisikiaje?
Migi: Naanza kwa kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kupata ushindi wa Kagame, pia nimekuja hapa nikiwa mchezaji mpya nikiwa sijazoeana na wachezaji wenzangu lakini nilijaribu kutumia uzoefu wangu nilionao nikajaribu kusaidiana na wenzangu na tumepata kombe nimefurahi sana.
Swali: Umeingia kwenye timu ya Azam na umeweza kucheza kwenye kikosi cha kwanza ukiwa hauna muda mrefu, nini siri ya mafanikio yako?
Migi: Sio kitu kingine ni kujituma sana, ukijituma zaidi na kufuata maelekezo ya kocha anayokuambia lazima utafanikiwa. Mimi naweza kusema kuwa, nilijaribu kuzoea haraka, nina uzoefu na kufuata anachoniambia kocha wangu Stewart.
Bofya hapa chini kumsikiliza Mugiraneza akieleza mwenyewe jinsi alivyoweza kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha AzamBofya hapa chini kumsikiliza Mugiraneza akieleza mwenyewe jinsi alivyoweza kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha Azam
0 Maoni:
Post a Comment