Sunday, September 20, 2015

AZAM FC PUNGUFU WAICHAPA MWADUI FC, WAFIKISHA POINTI 9

Posted By: kj - 6:49 PM

Share

& Comment

Azam FC leo imejiongezea pointi tatu baada ya kuifunga Mwadui FC 0-1 na kuendelea kukabana na Simba na Yanga kileleni mwa  msimamo  wa VPL kwa pointi tisa (9)

Goli la Azam FC leo limefungwa na nahodha wake John Bocco katika dakika ya 48 baada ya kukokota mpira na kuwazidi mbio mabeki wa Mwadui FC wakiongozwa na Joram Mgeveki kasha kufunga kiustadi.

Mchezo huo uliingia dosari kwa Azam FC muda mchache baada ya kupata goli baada ya beki wake tegemeo Aggrey Morris kupewa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi mshambuliaji wa Mwadui FC Rashid Mandawa na mwamuzi kuwapa Mwadui Penati ambayo ilipanguliwa na kipa wa Azam FC Aishi Manula.

Ingawa ni kweli Aggrey alicheza faulo, lakini kosa lile halikustahili kadi nyekundu kutokana na marekebisho ya sheria za soka. Ilikuwa sahihi kwa Mwadui kupata penati na Aggrey angepewa kadi ya njano. Kadi nyekundu na penati ni adhabu kubwa sana hasa kutokana na ukweli kwamba pembeni kwa Agrey kulikuwa na David Mwantika mwenye kasi aliyekuwa anakwenda kuingilia mchezo. Lakini Maamuzi ya refarii ndiyo ya mwisho na Azam FC inayaheshimu.

Baada ya kadi hiyo Azam FC ililazimika kufanya mabadiliko kwa kumtoa Kipre Tchetche na nafasi yake kuchukuliwa na Racine Diof .

Baada ya hapo Azam FC ilipunguza mashambulizi na kujaribu kulinda ushindi jambo ambalo walifanikiwa.

Pamoja na ushindi, Azam FC inaipongeza Mwadui FC kwa mchezo mzuri wa kuvutia na ushindani. Mwadui wana uwanja mzuri wa kuchezea soka, wana kikosi kizuri cha wachezaji wazoefu na wametoa ushindani unaolingana na ukubwa wa ligi kuu ya Tanzania.

Azam FC inarejea kesho jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mchezo dhidi ya wagonganyundo wa jiji la kijani kibichi, Mbeya City Council Authority

Kikosi cha Azam FC kilichoanza leo ni
Aishi Manula, Kapombe Shomary, Mwantika David, Agrey Morris, Pascal Wawa, Himid Mao, Salum Aboubakar/Mudathir Yahya, Domayo Frank Rymond, Kipre Tchetche/Racine Diof, John Bocco, Farid Mussa

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.