Katika mchezo wa leo ambapo Azam FC walianza na wachezaji wanne ambao hawakuwemo katika kikosi kilichopata ushindi dhidi ya Mbeya city na kufanikiwa kupata ushindi huo wa goli 2-0, ambapo magoli yote mawili yalifungwa katika kipindi cha pili.
Kama ilivyo ada Azam FC walianza mchezo kwa dhamira ya kupata goli la mapema lakini uimara wa kipa wa Coastal union ulichelewesha magoli ya Azam FC.
Katika kipidi hicho cha kwanza Azam FC walitengeneza nafasi chache za magoli kulinganisha na kipindi cha pili, huku umiliki wa mpira katika ukiwa sawa na muda mrefu ukichezwa eneo la kati ya uwnaja.
Katika kipnidi cha pili Azam FC walikuja kivingine kabisa na kucheza soka la uhakika na kutengeneza nafasi kadhaa za magoli.
Katika dakika ya 46 Shomari Kapombe aliiandikia Azam FC goli la kwanza akiunga mpira wa kona uliopigwa na Farid Mussa Maliki.
Dakika chache baada ya goli kuingia Azam FC walipoteza nafasi ya kuikiandikia goli la pili kupitia kwa Kipre Tcheche.
Katika dakika ya 55 kocha Stewart John Hall alimpumzisha Ramadhan Singano ambaye alikuwa ancheza mchhezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya vodacom akiwa na uzi wa Azam FC na nafasi yake kuchukuliwa na fundi Salum Abubakri Sure boy.
Kuingia kwa Sure boy kuliimarisha safu ya kiungo ya Azam FC na kupelekea kutawala eneo hilo, huku wakicheza soka la uhakika.
Katika dakika ya 70 kama ilivyo ada Salum Abubakari alimpikia goli Kipre Tcheche ambapo Tcheche bila ajizi aliiandikia Azam FC goli la pili, na kupelekea mchezo kumalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 2-0 na kufikisha pointi 15 sawa na yanga.
Azam FC leo: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Said Morad, Pascal Wawa, Racin Diouf, Farid Mussa Malik, Jean Baptist Mugereneza, Franky Domayo, Ramadhan Singano/Salum Abubakri, Allan Wanga/Didier Kavumbagu na Kipre Tcheche/Ame Ally
0 Maoni:
Post a Comment