Tuesday, September 29, 2015

AZAM WAMSHATAKI NYOSO TFF

Posted By: kj - 9:59 PM

Share

& Comment


Uongozi wa club ya Azam FC leo umewasilisha barua ya malalamiko yao kuhusu tukio la udhalilishaji alilofanyiwa mchezaji wao John Bocco na Juma Nyosso wa Mbeya City wakati wa mechi ya ligi kuu ya VodacomTanzania bara kati ya Azam FC dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, siku ya Jumapili Septemba 29.09.2015.

Barua hiyo yenye kumbukumbu namba TPLB/AZAMFC/01/15 imewasilishwa kwenye ofisi za TFF na afisa habari wa club hiyo Jafar Idd Maganga majira ya saa 6 mchana.

Jafar amesema, licha ya kuwasilisha barua yao ya malalamiko dhidi ya kitendo kilichofanywa na Nyosso, club ya Azam inalaani vikali kitendo hicho na kuiomba TFF kuchukua hatua za kinidhamu juu ya mchezaji husika.

“Baada ya Juma Nyosso kumfanyia  kitendo cha udhalilishaji mchezaji wetu John Bocco, uongozi wa Azam FC  umelaani vikali sana tukio hilo lililotokea wakati wa mchezo wetu dhidi ya Mbeya City na kuamua kuandika barua kwa Shisikisho la Mpira wa Miguu (TFF)”, amesema Jafar.

“Lakini sisi hatuingilii maamuzi ya TFF juu ya adhabu gani apewe Nyosso, wao kupitia kamati husika ya nidhamu, watatoa maamuzi yao kulingana na kanuni zinavyoelekeza”.

“Sisi kama Azam FC tumewakilisha barua TFF waweze kulifanyia kazi tukio hilo kutokana na vifungu ambavyo vimeanisha lakini narudia tena, hatuingilii majukumu ya TFF wao ndio wanajua ni adhabu ya aina gani ambayo inaweza kumkabili mchezaji huyo kutokana na kitendo ambacho amekifanya”.

Hii hapa chini ni barua ya Azam FC iliyowasilishwa leo kwenye shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF)

Chanzo: Shaffihdauda.co.tz

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.