Saturday, September 26, 2015

HALL: WANGA AKIWA FITI 100%, MTAISOMA NAMBA

Posted By: kj - 3:00 PM

Share

& Comment


KOCHA wa Azam, Stewart Hall amemwangalia straika wake, Allan Wanga na kubaini kuwa bado hajawa fiti kwa asilimia 100, lakini akasema mara atakapokuwa fiti basi mastraika wengine nchini wajiandae kusubiri.

Hall alisema kwa dakika chache pekee alizocheza, Wanga ameonyesha ni bonge la straika ambaye alistahili kabisa kusajiliwa Azam, hivyo akiwa fiti kucheza dakika 90 wapinzani wao lazima waisome namba.

Wanga amesajiliwa na Azam msimu huu baada ya kumaliza mkataba wake na El Merreikh ya Sudan. Awali, Azam ilikuwa ikimwania Mohammed Traore wa timu hiyo ya Sudan lakini dili lake lilipokwama ndipo ikamchukua Wanga.

“Wanga ni straika hatari sana, anajua lilipo goli na anafanya vizuri sana mazoezini na kwenye mechi licha ya kwamba bado hayupo fiti,” alisema Hall.

“Akiwa fiti itakuwa shida maana kasi yake na uwezo wake wa kufunga utakuwa juu, ameibua changamoto kubwa katika kikosi changu.”     


Chanzo: mwanaspoti

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.