Tuesday, September 8, 2015

MSENEGAL APEWA MWEZI MMOJA AZAM FC

Posted By: Unknown - 3:24 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa Kombe la Kagame, Azam FC iwamemsainisha mkataba wa mwaka mmoja beki wa kati Msenegali Ricene Diouf baada ya kocha mkuu wa kikosi hicho, Stewart Hall kuridhishwa na kiwango chake.

Matajiri hao wa Chamanzi wamekamilisha usajili wa mchezaji huyo mapema baada ya kumfanyia majaribio mazoezini na kwenye mechi za kirafiki na Stewart kuridhika na uwezo wake wa kumiliki mpira, kutoa pasi zenye uhakika, kukaba pamoja na uzoefu.

Azam imeimarisha safu ya ulinzi ambao kocha Stewart anapenda kutumia mfumo wa 3-5-2 wa wachezaji watatu nyumba, watano katikati na wawili mbele, ambapo Diouf ataungana na Muivory Coast Serge Wawa, Aggrey Morris, Said Morad, David Mwantika na Abdallah Kheri.

Hall aliliambia gazeti hili kuwa, tayari wamemsainisha Diouf mkataba wa mwaka mmoja.

“Ni mchezaji mzuri kwa kipindi kifupi tulichokaa naye, amefanya vizuri, ana uwezo wa kumiliki mpira, pasi zake zinafika kwa mlengwa, anajua kukaba na sifa kuu ana uwezo wa kucheza kwa ufasaha mguu wa kushoto mtu  ambaye nilikuwa namwitaji sana, hivyo ndiyo maana tumeamua kumpa mkataba wa mwaka mmoja,”alisema Stewart.

Katika hatua nyingine kipa wa zamani wa Simba, Ivo Mapunda ameanza mazoezi katika kikosi cha Azam. Hall alisema watakuwa na Ivo kwa kipindi chote lengo ni kumweka fiti kama wataafikiana na kiwango chake basi wanaweza kumsajili wakati wa dirisha dogo


Chanzo: mwananchi.co.tz

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.