Mcha alikuwa nje ya dimba kwa muda wa takribani miezi minne akiuguza majeraha ya goti lake la mguu wa kushoto, kabla ya kurejea dimbani alikuwa akifanya mazoezi na timu ya vijana ya Azam FC.
Alhamisi iliyopita alicheza mchezo wake wa kwanza msimu huu wakati Azam FC ilipoifunga Ndanda bao 1-0, akiingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ame Ally 'Zungu'.
"Nimefurahi sana kurejea uwanjani, nilikuwa naona wivu sana na kuumia nikiwaona wenzangu wanacheza na mimi nikiwa nje kwa majeraha, ni jambo jema sasa nimerudi na mimi napigania kurudisha kiwango changu na kuwa Mcha yule kabla ya kuumia," alisema Mcha akiuambia mtandao huu.
Mcha alisema furaha yake isingeweza kuisha haraka kama angefanikiwa kufunga bao kwenye mechi hiyo, huku akidai kuwa anachofanya hivi sasa ni kupambana kuhakikisha anarudisha kiwango chake na kurejeshwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'.
"Mimi napambana kurejesha kiwango changu kwanza, kama baadaye kocha Taifa Stars ataona nafaa, ataniita," alisema.
Winga huyo mzaliwa wa Zanzibar anasifika kwa uwezo mkubwa wa kupiga mipira ya adhabu ndogo, akiwa na historia ya kufunga mabao kadhaa ya aina hiyo na kutengeneza mengine
0 Maoni:
Post a Comment