Sure Boy amekiri kuwa msimu huu pia upo tofauti na msimu uliopita ambapo changamoto ya timu za juu ilikuwa zaidi kwa Yanga lakini sasa hivi hata Simba nao wameamka na wamepania kufanya kweli, hivyo kuzidi kuzidisha ugumu wa ligi hiyo na kuifanya isitabirike mapema.
Aidha, kuhusiana na mchezo wao wa wiki ijayo dhidi ya Wanajangwani hao, Sure Boy alisema ni mchezo mgumu na hawezi kutoa matokeo mapema kwa maana anajua Yanga wamejiandaa hivyo na wao watahakikisha wanakuwa vizuri kwa ajili ya kutafuta pointi tatu muhimu.
“Aisee, hii ligi ya safari hii ngumu sana, hata msimu uliopita haikuwa hivi, hii ya sasa haitabiriki maana kama unavyoona Yanga imeng’ang’ania kileleni na kila mchezo inashinda na kuzidi kutupa wakati mgumu, kwa sababu hata Simba safari hii nao wamejiandaa na wanashinda mfululizo, kwa hiyo hii inatupa wakati mgumu wa kutwaa ubingwa.
“Tutakapokutana nao, mechi haitakuwa nyepesi hata kidogo, wao wamejiandaa safari hii kama wanavyoonekana lakini hata na sisi pia tumedhamiria kuchukua pointi tatu katika kila mchezo, kwa hiyo tusubiri dakika 90,” alisema Sure Boy.
Yanga iliyo kileleni mwa msimamo wa ligi inatarajia kuumana na Azam wanaoshikilia nafasi ya pili Oktoba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
0 Maoni:
Post a Comment