Uongozi wa Azam FC, umethibitisha kuwa upo katika hatua za mwisho za kumsainisha aliyekuwa kipa wa Simba, Ivo Mapunda ambaye kwa muda sasa amekuwa akifanya mazoezi na kikosi hicho.
Mapunda aliachana na Simba mwanzoni mwa msimu huu, baada ya uongozi wa timu hiyo kukatisha mpango wa kumsajili licha ya kumkabidhi pesa zake za usajili.
Katibu Mkuu wa Azam FC, Idrissa Nassor, amesema wanatarajia kumsajili Mapunda katika usajili huu wa dirisha dogo, hivyo atakuwa ni mchezaji pekee atakayesajiliwa na timu hiyo kipindi hiki.
“Tupo katika hatua za mwisho za kumsajili Ivo, kwa sasa tupo kwenye mazungumzo ya kujua tutampa mkataba wa muda gani na mara baada ya kukubaliana, tutaweka hadharani kila kitu.
“Kwa upande mwingine, wachezaji wetu wote wapo vizuri na hakuna tutakayemuondoa kwa sasa,” alisema Idrissa.
CHANZO: SALEHJEMBE BLOG
0 Maoni:
Post a Comment