Saturday, November 7, 2015

MWEDA AJUMUIKA NA WANAFUNZI KUAZIMISHA SPORTS DAY

Posted By: kj - 12:46 PM

Share

& Comment

BEKI kisiki wa timu ya Azam FC, Said Morad ‘Mweda’, juzi alifanya mambo yanayofanywa na mastaa wakubwa duniani kutoka barani Ulaya.

Hiyo ni baada ya kucheza pamoja na kuwafundisha soka wanafunzi takribani 600 wa Kituo cha elimu cha ‘Master the Great Education Center’, waliotembelea viunga vya Azam Complex juzi na kuadhimisha siku yao ya michezo ‘Sports Day’.

Baadhi ya wachezaji kutoka Ulaya waliowahi kufanya mambo hayo ni pamoja na mastaa wa dunia Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo anayekipiga Real Madrid wakati huo akiwa Manchester United.

Wengine ni nyota wa zamani wa Arsenal na United, Robin van Persie, David Beckham (United, Real Madrid, AC Milan, LA Galaxy, PSG), kiungo wa Chelsea aliyewahi kukipiga Arsenal na Barcelona, Cesc Fabregas.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.