Saturday, January 16, 2016

AZAM FC WATOKA SARE NA AFRICAN SPORTS

Posted By: kj - 9:53 PM

Share

& Comment


Vinara wa ligi kuu ya vodacom Azam FC leo wamelazimishwa sare na African Sports ya Tanga katika mchezo uliochezwa leo usiku katika uwanja wa Azam complex na kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Katika mchezo huo uliomshuhudia beki Waziri Salum akicheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya vodacom toka katika msimu wa 2013/14 ambao aliumia na kumfanya awennje ya uwanja kwa takribani mika miwili.

Azam FC waliuwanza vyema mchezo huo na kutawala vilivyo katika kipindi cha kwanza na kupelekea African Sports muda mwingi wakiwa wanasaka mpira huku wakibakia katika eneo lao wakijiami.
Katika kipindi cha kwanza African sports walifanya majaribio mawili kwa kipa wa Azam FC ambapo jaribio moja liligonga mwamba na moja kuishia katika mikono ya Aishi Manula.

Azam FC waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 27 kupitia kwa Franky Domayo kwa shuti kali alilopiga nnje ya eneo la hatari.

Kuingia kwa goli hilo kulitengeneza mianya ya Azam FC kutenegeneza nafasi ambapo walishindwa kuzitumia nafasi hizo na kupeleka mchezo kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1.

Kipindi cha pili African Sports walirejea tofauti na kupelekea kutowapa nafasi ya Azam FC ya kuchezea mpira na kufanya mchezo kuwa sawa kwa upande zote mbili.

Katika dakika ya 58 Hamad Nidhania aliiandikia African sports goli la kusawazisha na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Kwa matokeo hayo yanapelekea Azam kuwa mbele ya yanga kwa pointi tatu ambazo endapo watapata ushindi kesho, watarejea kileleni kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.


MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM

RnTimuPWDLFAGdPts
1Azam FC1411302891936
2YANGA1310303052533
3SIMBA SC149322191230
4MTIBWA SUGAR14833179827
5STAND UNITED148151511425
6T. PRISONS147341414024
7MWADUI FC146441613322
8TOTO AFRICANS144551216-417
9MGAMBO SHOOTING144461214-216
10MBEYA CITY143561215-314
11JKT RUVU143381621-512
12MAJIMAJI FC14338924-1512
13Coastal Union14176815-710
14NDANDA FC13166915-69
15KAGERA SUGAR14239417-139
16AFRICAN SPORT142210415-118

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.