MCHEZO wa raundi ya 17 wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Azam FC dhidi ya Mwadui umesogezwa mbele siku moja na sasa utachezwa Jumatatu Februari 8, mwaka huu badala ya Jumapili.
Azam FC kwa sasa iko Zambia ikishiriki michuano maalumu, ambapo leo itacheza mchezo wa mwisho dhidi ya Zanaco FC kabla ya kurejea Dar es Salaam kesho.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Baraka Kizuguto alisema: “Kuna michezo mingine itaendelea mwishoni mwa wiki ijayo kwa timu nyingine isipokuwa Azam FC imepangiwa kucheza Jumatatu baada ya kurejea kutoka Zambia,”alisema.
Aidha, alisema timu hiyo itacheza mechi zake za viporo dhidi ya Prisons kuanzia Februari 24, mwaka huu na dhidi ya Stand United Machi 16, mwaka huu.
Kwa upande wa timu ya Yanga itacheza mechi na Stand United kabla ya kuanza maandalizi ya mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius.
Mchezo huo wa raundi ya awali unatarajiwa kuchezwa ugenini kati ya Februari 12,13 na 14 mwaka huu nchini humo na kurudiana kati ya Februari 26, 27 na 28, Dar es Salaam
Chanzo: Habari leo

0 Maoni:
Post a Comment