Mabingwa wa klabu bingwa Afrika mashariki na kati Azam FC, wamefanikiwa kuvuna pointi tatu mbele ya Stand united katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya Tanzania Bara.
Katika mchezo huo uliopaswa kuchezwa mwanzoni wa mwezi februari, ulishuhudia kipindi cha kwanza kumalizika bila kufungana, huku Azam FC wakitawala mchezo huo kwa kucheza pasi fupi fupi.
Azam FC walitengeneza nafasi tatu katika kipindi cha kwanza na kushindwa kuitumia huku Stand united wakitengenza nafasi moja ya wazi.
Kipindi cha pili kilirejea kwa kasi huku kila timu ikishambuliana kwa zamu na Azam FC kubadilisha aina ya uchezaji na kuanza kutumia mipira mirefu, wakati wa kupandisha mashambulizi.
Dakika ya 63 krosi ya mtokea benchi John Bocco, iliungwa vyama na Shomari Kapombe na kuindikia Azam FC goli la kuongoza.
Kuingia kwa goli hjilo kulipeleka Azam FC muda mwingi kuchezea mpira katika eneo lao, huku na marachache kutumia mipira mirefu kuwatafuta washambuliaji wao.
Stand united waliongeza kasi na kutengeneza nafasi mbili ambazo pia walishindwa kuzitumia na kupeleka mchezo kumalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 1-0, na kupunguza wigo wa pointi baina yake na kinara Simba SC.
MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM
Rn | Timu | P | W | D | L | F | A | Gd | Pts |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | SIMBA SC | 23 | 17 | 3 | 3 | 41 | 13 | 28 | 54 |
2 | YANGA | 21 | 15 | 5 | 1 | 51 | 11 | 40 | 50 |
3 | Azam FC | 21 | 15 | 5 | 1 | 37 | 13 | 24 | 50 |
4 | MTIBWA SUGAR | 21 | 11 | 6 | 4 | 26 | 14 | 12 | 39 |
5 | T. PRISONS | 23 | 9 | 9 | 5 | 21 | 20 | 1 | 36 |
6 | MWADUI FC | 23 | 9 | 7 | 7 | 22 | 19 | 3 | 34 |
7 | STAND UNITED | 23 | 9 | 3 | 11 | 19 | 21 | -2 | 30 |
8 | NDANDA FC | 22 | 5 | 9 | 8 | 19 | 23 | -4 | 24 |
9 | MBEYA CITY | 23 | 6 | 6 | 11 | 22 | 30 | -8 | 24 |
10 | MAJIMAJI FC | 23 | 6 | 6 | 11 | 13 | 32 | -19 | 24 |
11 | TOTO AFRICANS | 22 | 5 | 8 | 9 | 19 | 30 | -11 | 23 |
12 | KAGERA SUGAR | 23 | 5 | 7 | 11 | 17 | 25 | -8 | 22 |
13 | JKT RUVU | 23 | 5 | 6 | 12 | 23 | 33 | -10 | 21 |
14 | MGAMBO SHOOTING | 23 | 4 | 8 | 11 | 18 | 28 | -10 | 20 |
15 | AFRICAN SPORT | 23 | 5 | 5 | 13 | 9 | 26 | -17 | 20 |
16 | Coastal Union | 23 | 4 | 7 | 12 | 15 | 29 | -14 | 19 |
0 Maoni:
Post a Comment