Sunday, March 20, 2016

BIDVEST WACHAPWA NNJE NDANI, AZAM KUKUTANA NA ESPERANCE APRILI 10

Posted By: kj - 5:51 PM

Share

& Comment


Mshambuliaji wa toka wa Azam FC toka nchini Ivory coast ameongoza mauaji Azam FC hiii leo kwa Bidvest toka nchini Afrika kusini, katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Azam complex.

Katika mchezo huo wa leo Azam FC walicheza taratibu na katika dakika ya 23 waliandika goli la kwanza kupitia kwa Kipre Tcheche akimalizia akiunga kwa kichwa krosi ya Ramadhani Singano.

John Bocco aliiandikia Azam FC goli la pili akimalizia pasi murua ya Kipre Tcheche katika dakika ya 42, kalba ya Bidvist ya Afrika kusini kuandika goli lake la kwanza katika dakika ya 43 na kupeleka mchezo kwenda mapumziko Azam FC wakiwa mbele kwa goli 2-1.

Katika kipindi cha pili Bidvest ilirejea kwa kasi na kujaribu kutawala mchezo huku wakikabia kwa juu.

Katika dakika ya 55 Kipre Tcheche akiwazidi mbio mabeki wa Bidvest baada ya kupitishiwa mpira na Ramadhan Singano, na kumpangua kipa na kuiandika Azam FC goli la 3 katika mchezo huo wa kombe la shirikisho.

Dakika 4 baada ya kuingi kwa goli ilo Bidvest waliandika goli lao la pili kabla ya kocha Steawart Hall kumpumzisha Himidi Mao na kumuingiza Jean Mugereneza.

Alikuwa Kipre Tcheche akifunga goli lake la tatu likiwa ni la nne kwa Azam FC katika mchezo wa leo katika dakika ya 88, kabla ya Bidvest kufunga goli la 3 na kupeleak mchezo kumalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 4-3.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Azam FC kuiondosha mashindanoni Bidvest kwa jumla ya magoli 7-3, baada ya kuibuka na ushindi wa goli 3-0 katika mchezo wa awali na leo kuibuka na ushindi wa goli 4-3.

Kwa matokeo hayo Azam FC watacheza na Esperence ya nchini Tunisia katika mchezo wa raundi ya pili, utakaochezwa aprili 10 katika uwanja wa Azam complex kabla ya kurejeana nchini Tunisia aprili 19 mwaka huu.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.