NAHODHA wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’, amesema kuwa bado wataendelea kupambana katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Kombe la Shirikisho Afrika ili kutimiza malengo waliyojiwekea.
Azam FC inayodhaminiwa na Benki bora kabisa nchini ya NMB, imejiwekea malengo ya kutwaa ubingwa wa VPL msimu huu pamoja na kufika hatua ya makundi (robo fainali) ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu.
Mabingwa hao wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati (Kombe la CECAFA Kagame), mwishoni mwa wiki iliyopita waliitoa Bidvest Wits ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 7-3 kwenye raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika na sasa itakutana na Esperance katika raundi pili ya michuano hiyo.
Mchezo wa kwanza dhidi ya Esperance utafanyika Aprili 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam kabla ya ule wa marudiano kupigwa wiki moja baadaye jijini Tunis.
Katika VPL Azam FC inashika nafasi ya tatu ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 50 sawa na Yanga iliyo nafasi ya pili kwa tofauti nzuri ya mabao ya kufunga na kufungwa (GD), lakini inazidiwa mechi tatu za kucheza kama Yanga dhidi ya Simba iliyokileleni kwa pointi
Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu hii www.azamfc.co.tz mara baada ya kumalizika kwa mchezo uliopita dhidi ya Bidvest, Bocco aliwahakikishia mashabiki wa Azam FC kuwa watazidi kupambana hadi dakika ya mwisho na kuhakikisha timu hiyo inafika mbali zaidi kwenye michuano hiyo.
“Tunamshukuru Mungu tumeweza kuvuka na kwenda kwenye hatua nyingine, tunachowaahidi mashabiki wetu tutaendelea kupambana katika ligi pia michuano ya kimataifa na kufika mbele zaidi,” alisema.
Bocco amefunga jumla ya mabao mawili kwenye mechi zote dhidi ya Bidvest, akifunga moja jijini Johannesburg waliposhinda mabao 3-0 mengine yakitupiwa na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Shomari Kapombe, kabla ya nahodha huyo kupiga jingine walipowararua Wasauzi hao 4-3 ndani ya Uwanja wa Azam Complex, mchezo ulioshuhudiwa Kipre Tchetche akifunga hat-trick (mabao matatu).
0 Maoni:
Post a Comment