Hiyo inatokana na mvua kubwa kunyesha wakati timu hizo zikichuana kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ulioisha kwa sare ya bao 1-1, na kupelekea kuwepo kwa hali ngumu ya uchezaji kutokana na uwanja kuloa sana.
Akizungumza na mtandao wa klabu www.azamfc.co.tz Migi alisema mpaka sasa amecheza mechi nyingi za kimashindano, lakini mechi ya jana dhidi ya Toto imeingia kwenye historia yake ya soka kutokana na kucheza kwa mara ya kwanza kwenye mazingira magumu kama yale.
“Nashangazwa sana hapa Tanzania, mpira kuendelea kwenye mazingira kama yale, maji ya mvua yalijaa sana uwanjani na kufunika mistari ya vipimo vya uwanja, sisi kwetu Rwanda mechi kama ile ingeahirishwa na kuchezwa siku nyingine.
“Tulishindwa kabisa kupiga pasi kutokana na mpira kunasa kwenye maji kila tukifanya hivyo, niliwahi kucheza hivi Songea tulivyocheza na Majimaji, lakini kule maji hayakujaa na mpira ulikuwa ukienda, hata waamuzi nao walikuwa wabovu sana, sijawahi ona hali hii na kwa kweli hii mechi itabaki kwenye historia yangu,” alisema.
Nahodha Msaidizi huyo wa timu ya Taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, amekuwa nguzo muhimu kwenye eneo la kiungo wa ukabaji tokea alipojiunga na Azam FC Julai mwaka jana akitokea APR ya jijini Kigali alikozaliwa.
0 Maoni:
Post a Comment