Thursday, July 28, 2016

KIUNGO WA MEDEAMA KUTUA CHAMANZI

Posted By: kj - 9:05 AM

Share

& Comment

Wakati ikikabiliwa na hatari ya kumpoteza mchezaji mwingine kutoka Afrika Magharibi, Kipre Tchetche, Azam imenasa saini ya kiungo chipukizi wa Medeama, Enoch Atta Agyei na kumpa mkataba wa miaka miwili.

Mwananchi lilikutana na ofisa mtendaji mkuu wa Azam, Saad Kawemba mjini Takoradi ambaye hakusita kusema ukweli juu ya ujio wa kinda huyo.

Kawemba alisema waliwatazama vijana watatu katika kikosi cha Medeama kwa lengo la kumpata mmoja atakayeimarisha kikosi chao msimu ujao.

Alisema baada ya kujiridhisha na uwezo wa kiungo huyo mkabaji, wameamua kufanya naye kazi kwa muda huo wakati wakijipanga kurudi kwa kasi katika msimu mpya wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa. 

Chanzo: Mwananchi

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.