Wednesday, September 6, 2017

7000 KUSHUHUDIA AZAM WAKIANDIKA HISTORIA

Posted By: dada - 2:35 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Azam FC wanataraji kuweka historia mpya ya uwanja wao wa Azam complex siku ya jumamosi watakapo cheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Simba SC katika uwanja huo.

Katika kuelekea mchezo huo wa pili kwa kila timu katika msimu huu wa ligi kuu, tiketi za mchezo huo zimeanza kuuzwa kupitia SELCOM ambapo bei zake ni Tsh 7000 kwa mzunguko na Tsh 10000 kwa VIP.

Azam FC toka waanze kutumia uwanja wa Azam Complex haijawai kucheza na Simba SC wala na Yanga katika uwanja huo, na ni timu moja tu iliyofanikiwa kupata ushindi dhidi Azam FC katika uwanja huo ambayo ni JKT Ruvu iliyopata ushindi mara mbili.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.