Tuesday, June 28, 2011

Kipre, Mtambo wa magoli

Posted By: kj - 5:31 PM

Share

& Comment

"NIMEPANIA kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara ilinilipe deni langu kwa Azam FC." Kauli hiyo ni ya mtambo mpya wa mabao uliosajiliwa na Azam, aliyetoa cheche za Brice Hermann Kipre Tchetche.

Kipre aliwaacha hoi mashabiki wa soka nchini na hata kuchukuliwa na Azam baada yakung'ara na Ivory Coast iliyoshiriki kama timu mwalikwa kwenye Kombe la Chalenji. Tchetche, ambaye alishika nafasi ya pili kwa ufungaji bora kwenye michuano hiyo, alikosha mashabiki kutokana na mara nyingi kuingizwa kipindi cha pili na kocha wa Ivory Coast, Kouadio Georges na kila mara kuzamisha bao.

Tchetche kwa umbo ni mnene na mfupi, ambaye unaweza kumfananisha na mshambuliaji hatari wa Manchester United na England Wayne Rooney. Mshambuliaji huyo mwenye sifa ya mbio na mashuti makali, alimaliza Chalenji akiwa na mabao manne nyuma ya Felix Sunzu wa Zambia aliyemaliza na matano. Alitoa mchango mkubwa kwa timu yake na kufika fainali na kulizwa na Tanzania Bara 1-0. Uwezo huo ndiyo uliwavutia Azam na kuamua kumsajili kwa ajili ya msimu ujao.

Azam kwa sasa ndio klabu inayoendeshwa kisasa zaidi nchini na hivi sasa inakamilisha kituo chake cha michezo kwenye eneo la Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Tchetche katika kikosi cha Ivory Coast, alikuwa na pacha wake Wilfred Kipre Bolou, ambaye ni kiungo mshambuliaji. Msimu uliopita, Tchetche aliibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Ivory Coast msimu uliomalizika, akiichezea Jeunesse Clubd'Abidjan na tangu ajiunge na Azam FC amekuwa akingara na kumfanya kocha wake, Stewart Hall asifu uwezo wake.

Pamoja na yote Kipre, ambaye amejazia misuli kwa mazoezi ana nguvu na kasi uwanjani, amejikuta katika wakati mgumu kwa kutokana na kufahamu lugha moja ya Kifaransa. Ikumbukwe Ivory Coast ni nchi iliyotawaliwa na Wafaransa na hata wakati fulani ilikuwa inahesabiwa kama jimbo la nchi hiyo na mwakilishi wao kwenye bunge la Ufaransa alikuwa muasisi wa taifa hilo, Felix Houphet Boigny. Tchetche anajitahidi kwa sasa kujifunza Kiingereza na kuzungumza maneno machache ya Kiingereza na Kiswahili.

Mwanaspoti ilimtafuta na kufanya naye mahojiano ilikufahamu malengo aliyonayo, alipotokea, mafanikio na matatizo yake kwa ujumla na yeye hakusita kueleza.

UJIO WAKE AZAM
Ni mwanasoka wa kwanza kutoka Ivory Coast kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwani wanasoka wengi wa huko wamekuwa na masoko katika nchi za Ulaya na mfano ni Didier Drogba anayechezea Chelsea ya England. Alipoulizwa kwanini hakutaka kuelekea Ulaya sawa nawenzake, Tchetche alijibu;��Hilo ni swali zuri sana, Azam FC sikuijua hapo awali, lakini ni bahati tu na Mungu ndiyo amenifikisha hapa, wao walinifuata wakinihitaji, ndiyo mimi na wakala wangu, ambaye ni kaka yangu Kipre Oscar Patrick tuliwafuatilia tukafahamu wana programua ya kuendeleza soka nikaipenda,��anasema Kipre, ambaye anayeishabikia Real Madrid ya Hispania na Manchester United ya England.��
Nimegundua Azam inamipango endelevu na naahidi kuichezea kwa mafanikio kwani naamini ndiyo timu itakayonipa mafanikio kwenda klabu kubwa Ulaya,��anaeleza Kipre aliyeitumikia JCAT kwa miaka mitano iliyopita bila kuhama na Azam ndiyo klabu yake ya kwanza kucheza nje ya nchi yake.

Anaeleza kuwa; Sikufanikiwa kupata timu kubwa Ulaya kutokana na kukosa bahati maana kila mafanikio yanatokana na bahati, lakini sasa naamini ni zamu yangu nitafanikiwa tu, lakini pia sikuwa na wakala wakunitoa, sasa nimepata naamini naweza kufika huko, ninacho takiwa ni kujituma nakucheza kiwango cha juu bila kuchoka.�

AHADI YA MABAO KWA AZAM
Anasema kama alikuwa anaingia kwa dakika chache kwenye Chalenji, lakini alifunga mabao, anaamini akiwa na Azam yataongezeka zaidi kwa sababu katika klabu aliyotoka ya JCAT, alikuwa anaichezea dakika 90 na kuwafungia mabao mengi.��

Azam wanataka ubingwa na ndiyo maana niko hapa, fahamu kuwa ubingwa hauji hivi hivi, ubingwa unatokana na mabao, tunatakiwa kufunga mabao mengi kwa kila mechi.��Ahadi ya mabao ndiyo ninayowapa mashabiki wa Azam FC, nitafunga mabao mengi kadri ya uwezo wangu kikubwa nahitaji ushirikiano, nafurahi pia tangu nifike naishi na wenzangu vizuri,��anasema Kipre.

TATIZO LA LUGHA�
Hilo ni tatizo mhh!�.. ni kweli mawasiliano yana nisumbua sana kwa sababu nazungumza kwa ufasaha lugha moja ya Kifaransa, Kiingereza changu ni kibovu ni kazi kunielewa na Kiswahili ndiyo hivyo ndiyo maana sipendi kuzungumza na watu.��Inanipa shida, lakini si sana kwa sababu tunaelewana, hata uwanjani kocha wangu namuelewa bila shida kwasababu lugha ya mpira (footballLanguage) ni moja, hakuna tofauti,�� anasema Kipre anayejifunza Kiingereza na Kiswahili kwa kutumia kompyuta ndogo (lap top) akitafsiri maneno yanayomshinda.

CHAKULA
Kipre anasema chakula cha Tanzania na Ivory Coast ni sawa, lakini mapishi yanatofautiana na chakula anachokula kinampa taabu: ��Chakula ni hicho hicho, kama ni wali, chapati, kuku, samaki na ugali pia nyumbani tunakula, lakini mapishi ya vyakula hivyo wanavyopika hapa vinatofautiana.��Napata taabu, lakini kidogo kidogo nazoea,��anaongeza Kipre, ambaye ameweka wazi kuwa anapendelea chapati na mchuzi.

HISTORIA YAKE
Kipre mwenye miaka 23, katika familia yao wamezaliwa watoto sita, watatu ni wanaume na watatu ni wanawake, kisoka yeye na kaka yake Kipre Bolou ndiyo wanacheza mpira na wengine wanajishughulisha na mambo mengine.

Ni baba wa mtoto mmoja wakike, mwenye miaka miwili anaitwa Kipre Astride na hajaoa, lakini anamchumba anaye tarajia kufunga naye ndoa.��Familia yetu ni ya soka kwasababu mimi na pacha wangu Bolou si unamjua yule ndiyo tunacheza mpira, lakini wengine wanajishughulisha na mambo mengine,�� anaongeza Kipre anayevutiwa na soka la Rooney na Raul Gonzalez Blanco wa Real Madried.

__________
BRICE HERMANN KIPRE TCHETCHE
Amezaliwa: Desemba 16, 1988,
Mahali: Abidjan, Ivory Coast.
Klabu: Jeunesse Club d'AbidjanTreicheville (JCAT) 2006-2011, Azam FC 2011-.
Taifa: Ivory Coast.


copied from mwanaspoti

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.