Saturday, June 25, 2011

Nafiu, Wahab watua kuanza kazi

Posted By: kj - 7:57 AM

Share

& Comment

Wachezaji wa Azam fc waliosajiliwa toka kwenye klabu ya Kingfaisal ya Ghana na raia Waghana, Nafiu Awudu na Yahya Wahab wali wasili jana alasiri.

Wachezaji hao walituwa jana saa tisa alasiri na shirika la ndenge ya Fly Emirates, wakitanguliwa na CEO wa Kingfaisal kukamilisha usajili wao, ambao ulikamilishwa hiyo jana. Kuwasili kwa Waghana hao kuna kamilisha wachezaji wa kigeni wa Azam FC kutua nchini kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu ya vodacom, inayo tarajiwa kuanza hapo agust 20.

Wachezaji wote wawili wanachezea timu ya vijana chini ya miaka 23 ya taifa la Ghana, huku Nafiu Awudu akicheza pia katika timu ya wakubwa Black Stars. Nafiu alikuwa nahodha wa kikosi cha Kingfaisal pamoja na kikosi cha Ghana cha wachezaji wanao cheza katika ligi za ndani. Abdul Wahab Yahya alishika nafasi ya tatu katika ufumaniaji wa nyavu kwenye ligi kuu ya Ghana.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.