Timu ya Azam Academy inayoshiriki mashindano ya Rolling Stone jana ilitinga hatuaya robo fainali ya mashindano hayo baada ya kuifunga timu ngumu ya TST toka Mwanza 1-0 shukrani kwa goli la Mange Chagula dk 35.
Ushindi wa jana ulikuwa muendelezo wa ushindi katika mashindano yanayoendelea ya Rollingstone jijini Arusha baada ya juzi kuifunga JKT Oljoro 2-1 katika mchezo wa hatua ya makundi ya mashindano hayo yanayoandaliwa na kituo hicho cha kukuza na kuendeleza michezo.
Azam Academy walianza mechi ya kwanza ya ufunguzi kwa kuifunga CIDT ya Arusha 4-0, kikosi hicho kitashuka uwanjani kucheza mchezo wake wa nne na wa mwisho leo kukamilisha ratiba na mwalimu wa timu hiyo Vivek Nagul ameuhakikishia mtandao wa klabu kuwa watahakikisha wanashinda pia mchezo wa leo. Mechi ya juzi magoli ya Azam yalifungwa na Joseph Kimwagana Ibrahim Rajab Jeba.
Azam Academy imefunga magoli saba na kufungwa moja katika michezo yote mitatu na kufiisha pointi tisa, haijatoka sare mchezo wowote. Azam watamaliza mchezo wa hatua ya makundi leo itakapocheza na timu ya kutoka nchini Burundi.
Akizungumza na tovuti ya www.azamfc.co.tz manager wa Academy Philip Alando amesema timu inaendelea vizuri na mechi zake, wachezaji wanapata uzoefu zaidi kwani timu nyingi zina wachezaji walio wazidi umri na wenye uzoefu wa mashindano hayo. Amesema katika mchezo wa jana walimkosa mshambuliaji mahiri Cosmas Lewis aliyepewa kadi nyekundu katika mchezo wa juzi, lakini anaamini wachezaji wengine wanaweza kucheza vizuri na kuziba pengo hilo.
Cosmas Lewis aliifungia timu yake magoli mawili katika mchezo wa kwanza dhidi ya CIDT iliyopata ushindi wa 4-0, magoli mengine yalifungwa na Ibrahim Jeba.
Copied from azamfc.co.tz
Friday, July 15, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment