Wednesday, July 27, 2011

Wahab atikisa nyavu

Posted By: kj - 10:12 PM

Share

& Comment

Maandalizi ya ligi kuu yana kwenda vizuri upande wa Azam FC baada ya leo kuifunga Moro United 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Azam Stadium jijini Dar es Salaam.

Moro United na Azam FC zikiwa katika matayarisho ya kabla kwa ajili ya ligi kuu ‘Pre season’ wamecheza mchezo huo kuvipa mazoezi vikosi vyao na kujiweka sawa kwa ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Octoba 20 mwaka huu. Azam FC wakiwa na mabadiliko katika kila mechi, walipata goli la kwanza dakika ya 36 kupitia kwa mshambuliaji wake mahiri Wahab Yahya aliyetokea nchini Ghana, goli ambalo limempa matumaini mshambualiaji huyo mwenye kasi na uwezo mkubwa awapo uwanjani.

Moro United walionyesha cheche zao wakiwa na kikosi kipya lakini hawa kuweza kuushinda uwezo wa wapinzani wao, dakika nane baadae mchezaji kinda Ibrahim Rajab ‘Jeba’ aliandika goli la pili katika dakika ya 44 akiunganisha krosi ya Wahab Yahaya. Goli la Jeba lilizipeleka timu zote mapumziko huku Azam FC wakiwa mbele kwa 2-0, kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko kuwapa nafasi wachezaji wao nafasi ya kucheza ili kujua uwezo wao.

Mchezo wa kipindi cha pili ulikuwa mgumu kwa pande zote, Azam FC wakiendelea kuutumia vyema uwanja wao walicheza mpira wa taratibu ukiwa na mashambulizi ya mara kwa mara kama ilivokuwa kwa Moro United.

Wachezaji Hilary Bingwa, Jerome Lambele, George Mkoba na Ally Msigwa walitoa mashambulizi lakini hawakuweza kupata goli na kupelekea dakika ya 88 ya mchezo kiungo Jabir Aziz alihitimisha mchezo huo kwa kufunga goli la tatu kwa kichwa akiunga krosi ya nahodha Ibrahim Shikanda.

Akizungumza baada ya mchezo kukamilika kocha wa Moro United, Hassan Banyai amesema mchezo ulikuwa mzuri, timu yake imepoteza mchezo huo kwa kuwa Azam FC walikuwa katika mazoezi ya muda mrefu pia ameridhika na kiwango cha wachezaji wake. “wachezaji wote wamejitahidi lakini mabeki wa kushoto walionekana mwanya kwa Azam hilo ni tatizo dogo, tukilirekebisha tutakuwa na timu nzuri zaidi.” Amesema Banyai.

Azam FC, Obren/Mwalami, Shikanda, Nyoni,/Jeba, Nafiu/Kakolaki, Humud, Mwaipopo/Sure, Bocco/Malika, Chombo/Jabir, Aggrey na Wahab.



copied from azamfc.co.tz

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.