Azam Football Club leo jioni itashuka kwenye uwanja wa Nakivubo jijini kampala kukwaana na SC Villa Jogoo katika mchezo wake wa pili wa maandalizi ya ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2011/12 hapa Kampala.
Katika mechi iliyopita dhidi ya Bunamwaya, Azam FC ilifungwa 4-3 huku magoli matatu ya bunamwaya yakifungwa ndani ya dakika 15 za kipindi cha kwanza.
Azam FC ambayo imezoea kufanya mazoezi kwenye uwanja wa plastic pale Azam Stadium ilipata taabu sana kuzoea uwanja uliojaa matope na wakati wakipambana na hali ya uwanja walijikuta wakiwa nyuma kwa magoli 3-0 na baadaye Bunamwaya kuongeza la nne, Lakini baadaye timu ilitulia na kucheza soka safi na kufanikiwa kufunga magoli matatu na hadi mwisho matokeo yakasomeka 4-3.
Azam FC iliyopo katika ziara ya mazoezi hapa kampala leo inacheza na SC Villa na kesho itashuka tena dimbani kukwaaana na Kampala City Council (KCC) kabla ya kumalizana na Victors FC hapo jumapili.
Hapo jana timu imefanya mazoezi katika uwanja wa Buziga Islamic Institute uwanja ambao hali yake hautofautiani sana na Nakivubo na kocha mkuu Stewart Hall alikuwa akiwafundisha vijana wake namna ya kucheza kwenye viwanja vibovu.
Ikumbukwe kuwa kwenye mechi nane za majaribio ambazo Azam FC imecheza, haijafanikiwa kushinda mchezo hata mmoja kwenye viwanja vibovu. Azam FC ilifungwa 2-0 na Coastal Union pale mkwakwani, ikatoka sare ya 0-0 na Zanzibar Select pale Mao TseDung Unguja kabla ya kufungwa 4-3 na Bunamwaya Nakivubo Stadium.
Azam leo itajaribu kushinda dhidi ya Villa ili kuondoa dhana kuwa timu haiwezi kushinda kwenye viwanja vibovu. Kwa mara ya kwanza leo mwalimu Stewart Hall amechagua wachezaji ambao anadhani wanafaa kucheza kwenye uwanja mbovu na kocha mkuu anajaribu kutengeneza Combination ya wachezaji watakao kuwa wakianza mechi za viwanja vizuri na wale watakaoanza mechi za viwanja vibovu.
Pia mfumo wa uchezaji leo utabadilika ambapo Ramadhani Chombo Redondo amerudishwa kwenye kiungo ambapo atacheza na Jabir Aziz huku Abdulhalim Humud akicheza kama Holding peke yake. Himid mao ambaye alicheza vizuri sana mechi iliyopita leo atapumzika lakini mwalimu amesema Himid atakuwa na nafasi kubwa na kuingia endapo mmoja kati ya viongo watatu aliopo uwanjani atacheza vibaya.
Kikosi kitakuwa kama ifuatavyo.
1. Mwadini Ally Mwadini
2. Ibrahim Shikanda
3. Waziri Salum Omar
4. Aggrey Morris
5. Said Morrad
6. Abdulhalim Humud Mohammed
7. Jabir Aziz Stima
8. Ramadhan Chombo Redondo
9. John Bocco
10. Kipre Tchetche
11. Mrisho Ngasa
azamfc.co.tz
Thursday, August 11, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment