Kwa mara ya kwanza hii leo Azam FC wamepoteza katika uwanja wake wa nyumbani wa Azam pale walipo wakaribisha wanambagala wa African Lyon.
Azam FC waliuwanza vyema mchezo huo nakupoteza nafasi ya kutikisa nyavu katika dakika ya 6 kupitia kwa John Bocco 'Adebayor' ambapo shuti lake lilichezwa vyema na Kipa wa African Lyon.
Azam FC walipeleka mashambulizi yake katika lango la African lyon kupitia upande wakulia ulikuwa na kapteni Ibrahim Shikanda, Mrisho Ngassa pamoja na Ramadhani Chombo aliyengara vilivyo huku akionekana kuegemea upande wa kulia na hivyo kuifanya African lyon kupeleka mashambulizi ya kushtukiza.
Hadi wanakwenda mapumziko milango ilikuwa migumu kwa pande zote mbili. Kipindi cha pili kilianza kwa Azam FC kupoteza nafasi kupitia kwa John Bocco baada ya mpira wake kugonga mwamba katika dakika ya 50.
Azam FC walipata pigo katika dakika ya 75 baada ya kiungo Salum Abubakari 'Sure Boy' kuzawadiwa kadi nyekundu na hivyo mchezo kubadilisha muelekeo na Azam FC kulemewa na mashambulizi ya African lyon.
Alikuwa ni Adam Kingwande aliyetibua rikodi ya kutofungwa ndani ya Azam Stadium na kucheza mechi 5 bila kupoteza. Kingwande aliandika bao hilo katika dakika ya 82 ya mchezo huo akiunganisha vyema krosi ya Agostino. Hadi mwisho wa mchezo Azam FC 0-1 African lyon.
Tuesday, August 23, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment