Wednesday, August 31, 2011

Azam waendelea kujifua

Posted By: kj - 4:43 PM

Share

& Comment

Wakati ligi ipo katika mapumziko ya siku 14, Azam FC wameendelea na mazoezi ya kujiweka sawa kwa kufanya mazoezi ya gym na uwanjani.

Hapo juzi Jumatatu, Azam FC ilifanya mazoezi ya nguvu katika viwanja vyake vilivyopo Chamazi Jijini DSM. Azam FC inatarajia kucheza mchezo wake wa tatu wa ligi kuu dhidi ya JKT Oljoro, utakaochezwa Jumatano ijao kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Katika mazoezi ya juzi Azam FC walifanya mazoezi ya kujenga mwili ‘gym’ kwa dakika 50, mazoezi maalumu ya kuongeza nguvu na kuweka misuli sawa kwa ajili ya michezo ijayo. Baada ya mazoezi hayo wachezaji walirejea uwanja na kuanza kufanya mazoezi ya kucheza na mpira pamoja na kucheza mechi ya dakika 45 mechi ambayo kila mchezaji alicheza.

Mazoezi ya leo yalihudhuriwa na wachezaji wachache ukiondoa watano waliopo timu ya Taifa, Mrisho Ngassa, Aggrey Moris, Jabir Aziz, John Bocco na Ramadhan Chombo, wachezaji wengine wote walikuwepo uwanjani lakini baadhi yao walikuwa na adhabu hivyo kufanya kundi lililokuwa kwenye programu kuwa dogo.

Wachezaji Abdulhalim Humud, Erasto Nyoni, Malika Ndeule, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ na Zahor Pazi, walichelewa kuingia katika uwanja wa mazoezi hivyo kocha Stewart Hall aliwapa adhabu ya kutofanya mzoezi iliwajirekebishe.

Akizungumzia kosa la wachezaji hao, kocha Stewart alisema ameamua kutoa adhabu hiyo iliiwe fundisho kwa wachezaji wengine, kwa kuwa sasa timu inahitaji umakini ‘seriousness’ katika kila kitu kwa kuwa inakabiliwa na michezo migumu pia wameshapoteza mchezo mmoja.

“Baada ya mchezo uliopita tulikaa na wachezaji wote tukazingumza na kukubaliana kuwa kila mmoja awe makini na kazi kuanzia mazoezini na katika jitihada binafsi ili kufikia malengo yetu, lakini baadhi wanaonesha kutojali, hivyo kuwekana sawa lazima wapatiwe adhabu” alisema Stewart.

Kocha ameongeza kuwa timu itaendelea na mazoezi hadi siku ya Jumapili kabla ya kuelekea Arusha siku ya Jumatatu kwa ajili ya mchezo huo. “Nasubiri wachezaji waliopo timu ya Taifa ili tuondoke pamoja, sipendi kusafiri na wachezaji wakiwa katika makundi tofauti ndiyo maana tumesubiri hadi Jumatatu watakapo kamilika tuanze safari ya pamoja” alisema Stewart.


azamfc.co.tz

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.