Azam FC jana jioni walikuwa visiwani Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa kirafiki ambao uliisha kwa sare ya bila kufungana.
Katika mchezo huo uliwagharimu Azam FC kumaliza wakiwa pungufu, baada ya kiungo mahiri Ramadhani Chombo 'Redondo' kuzawadiwa kadi nyekundu katika dakika ya 17 ya mchezo.
Azam FC itarejea leo jijini Dar es salaam, wakitokea visiwani Zanzibar. Kesho watapimana ubavu na JKT Ruvu katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi.
Katika hatua nyingine, ratiba ya ligi kuu Tanzania bara (VPL) imetoka jana huku Azam FC wakifungua ligi kwa kukutana na Moro United katika uwanja wa Azam.
Wednesday, August 3, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment