Kikosi kazi cha Azam FC jana kiliibuka na ushindi wa magoli matatu kwa bila katika uwanja wa Amahoro walipo wakabili Kampala City Council (KCC) uliochezwa jana.
Katika mchezo huo ambapo Wahab alishindwa kumaliza mpambano baada ya kuumia, kocha Stewart Hall alibadili kikosi kizima kilicho wakabili SC Villa.
Ilikuwa ni siku njema kwa kijana toka Zanzibar Khamis Mcha Vuai baada ya kuingia nyavuni mara mbili na kufikisha magoli 7 katika mechi 6 alizoteremka uwanjani na uzi wa Azam FC. Vuai alifungua ukurasa wa mabao katika kipindi cha kwanza na kurudi tena nyavuni kipindi cha pili.
Kipre Tchetche aliendeleza kumwaga cheche zake katika mechi za kirafiki kwa kukamilisha idadi ya magoli kwa Azam katika siku hiyo ya jana.
Azam FC walimaliza mpambano huo kwa ushindi wa goli 3 kwa bila. Azam watateremka tena katika uwanja huo hapo kesho kuwa vaa Victor ya Uganda kabla ya kuelekea Kigali kukamilisha ziara yake ya mechi za kirafiki.
Saturday, August 13, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment