MRISHO Ngassa wa Azam FC ametabiri kuwa msimu huu ndio mwisho wa ngebe na tambo za Simba na Yanga ambazo zimekuwa zikipokezana nafasi mbili za juu kila mara.
Azam imewasajili washambuliaji Kipre Tcheche wa Ivory Coast na Mghana Wahabu Yahaya kuongezea nguvu kikosi hicho kilicho maliza nafasi ya tatu msimu uliopita. Mbali na hao pia kuna mafowadi wazalendo kama John Boko na Ngassa ambaye atajiunga na Seattle Sounders ya Marekani Februari mwakani.
"Timu yetu msimu huu iko moto sana nafikiri kila moja ameiona, inawachezaji wote wazuri kuanzia mabeki, viungo na washambuliaji na wote wanafanya kazi kubwa uwanjani hivyo ligi itakuwa kali sana. Utawala wa Simba na Yanga utakoma ligi ikianza, ni mwendo wa kazi tu kuhakikisha nafasi mbili za juu tunashika mojawapo, kwani wao waweze wana nini na sisi tushindwe tunanini, hivyo watu wasubiri kuona, tutafunika sana," alisema Ngassa ambaye aliweka rekodi ya Mtanzania wa kwanza kucheza dhidi ya Manchester United ya England.
Timu hiyo itafungua pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kucheza na Moro United kwenye uwanja wao uliopo Chamazi, Mbagala.
Copied from mwanaspoti.co.tz
Saturday, August 13, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment